Friday, July 05, 2013

FANS WANGU WENGI WAMENISHAURI NIMWAMBIE MUME WANGU AACHANE NA SIASA, NA HUU NI MSIMAMO WANGU

Hapa kuna swala nahitaji kuliweka sawa, naamini tutaelewana fans zangu wote.


My Hubby Henry Kilewo.


My Hubby Henry Kilewo akiwa katika shughuli zake za kisiasa.


Nimeolewa na mwanasiasa, mume wangu Henry Kilewo ni katibu wa CHADEMA mkoa wa Kinondoni, Ila mimi si mwanasiasa(nahudumia watu wote wenye vyama na wasio na vyama).


Our Wedding Day, Nikila kiapo, "KWA TABU NA RAHA"

Muda nakubali kuolewa naye nilifahamu fika kuwa yeye ni mwanasiasa, Ila nitamsupport mume wangu kwa kazi yake aliyoichagua, siwezi kumwambia AACHE SIASA, Hilo kwa kweli HALIWEZEKANI, Hata yeye hajawahi hata siku moja kuniingilia katika kazi yangu ya kutetea haki za wanawake na maendeleo ya wanawake kwa ujumla(WANAWAKELIVE) na kuniambia niiache.


Hubby Henry Kilewo kikazi zaidi.

Ila nina swali la kuuliza hapa "KILA MTU ANAPOPATA TATIZO KATIKA KAZI YAKE ANATAKIWA KUIACHA???" Mfano Daktari akipata tatizo katika kazi yake aache? Ama Mwalimu ama mtu yoyote yule kwa kazi anayoifanya akipata changamoto anatakiwa kuacha????


My family, Hubby Henry With Our Boys, Lincon na Linston.

Fans Wangu wote naamini mtakuwa mmenielewa na mtaendelea kuwa nami all the way, Msimamo wangu ni huu, Nitasimama upande wake na kuendelea kumsupport mume wangu Henry, SIASA ni kitu anachokipenda SIWEZI KUMWAMBIA AACHE.

4 comments:

 1. Uko sawa kabisa dada Joyce. Nakussuport asilimia zote. Big up sana

  ReplyDelete
 2. And that's what we need in our society so don't be descouraged to that coz thats all the challenges in life and believe that he will be out of the court as soon coz the issue is to abolish CDM party from politics and that's all will not succeed through our prayer. Lastly big up for u are tolerance and cooperation to him as he is u are husband and we shall keep on praying to them and the advocates to defeat for all evils.

  ReplyDelete
 3. Huwezi kuwa shujaa kama hujapita kwenye changamoto. Mungu ameshawashindia. Nazidi kukuombea ww na family yako kwani Mungu wetu alituahidi kuwa Kila jaribu litupatalo linalingana na Imani yetu so usifadhaike kwa haya unayopitia sababu hakuna jaribu lisilo na mlango wa kutokea. Mungu wetu akubariki.

  Joyce M.
  Lusaka.

  ReplyDelete
 4. Kuna watu ambao hutoa ushauri bila kufikiria. Kama yeye ameamua kutetea haki za wananchi mwacheni ndo anachopenda kufanya. Huwezi mbadilishe yeye kwa kuwa anakutana na vikwazo mbalimbali....

  ReplyDelete

Toa maoni yako, epuka lugha ya matusi!

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...