Saturday, September 28, 2013

TANGAZO: WANAWAKELIVE TUMEHAMIA HUKU - WWW.WANAWAKELIVETV.COM

Tutoa taarifa rasmi kwamba sasaivi ukitaka kujua habari za wanawakelive kwa undani, usisite kutembelea website yetu mpya ya www.wanawakelivetv.com

Tunaomba radhi sana kwa usumbufu utakaojitokeza

Friday, September 27, 2013

VIDEO:WATOTO WANAPOPANGA KUPATA WATOTO, HILO NALO NI TATIZO.

Vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo katika jamii yetu, nikiwa huko mkoani Dodoma nilipata kushuhudia ndoa ya watoto wadogo kabisa, kiukweli nilikuwa nashangaa na bado nashangaa mpaka sasa hata siamini, haya nilikuwa nikiyasikia tu ama kuyasoma ila nimepata kuyaona kwa macho yangu.. mdau tutazame then tuje kuchangia mawazo mana inabidi ifike muda vitendo hivi vya ukatili wa kijinsia iwe vimefika mwisho...

VIDEO: BALOZI MWANAIDI MAAJAR "DAWATI KWA KILA MTOTO" KAMPENI INAYOENDESHWA NA TAASISI YA HASSAN MAAJAR.

Taasisi ya Hassan Maajar iliyoanzishwa kwa dhumuni kubwa la kusaidia elimu hapa nchini kwetu, leo imeandaa dinner pale Diamond Jubilee VIP Hall kwa ajili ya kuchangisha pesa itakayosaidia kununulia madawati kwa ajili ya shule zetu hapa nchini.. Kila mdau ana nafasi ya kushiriki kwa kununua meza.
Tusupport kampeni hii ili kuwapa mazingira mazuri ya kusomea watoto wetu, inawezekana!!!

MUSWADA WALETA KASHESHE...WENGI WAUKATAA

Muswada umeleta kasheshe, wengi wameukataa, wengi wanaume kwa wanawake wamemuomba Raisi asitie saini.

Thursday, September 26, 2013

VIDEO: WATOTO WAOANA...NA WAO WANAPANGA KUPATA WATOTO.

Vitendo vya ukatili wa kijinsia bado vipo katika jamii yetu, nikiwa huko mkoani Dodoma nilipata kushuhudia ndoa ya watoto wadogo kabisa, kiukweli nilikuwa nashangaa na bado nashangaa mpaka sasa hata siamini, haya nilikuwa nikiyasikia tu ama kuyasoma ila nimepata kuyaona kwa macho yangu.. mdau tutazame then tuje kuchangia mawazo mana inabidi ifike muda vitendo hivi vya ukatili wa kijinsia iwe vimefika mwisho...

Wednesday, September 25, 2013

MH BATILDA BURIANI AONYESHA ROHO YA KUJALI KWA KUCHANGIA DAMU KWA WAHANGA WA WESTGATE NCHINI KENYA.


Balozi wa Tanzania nchini Kenya Mhe Batilda S. Burian,  jana ameongoza umati wa Watanzania waishio Nairobi, Kenya,  kujitolea damu kwa ajili ya kuwasaidia waathirika wa tukio la ugaidi la kusikitisha lililotokea katika Westgate Mall tarehe 21 mwezi huu jijini Nairobi Kenya, ambapo hadi sasa zaidi ya watu wapatao 62 wameripotiwa kupoteza maisha na wengine zaidi ya 179 wamejeruhiwa vibaya na wengi wao bado wanaendelea kupata matibabu katika hospitali za Aga Khan University Hospital, Nairobi Hospital na Hospitali ya MP Shah.

Katika tukio hilo pia Mtanzania, Bwana Vedastus Nsanzungwanko, Meneja, Child Protection, UNICEF ni mmoja wa wale walioathirika na tukio hilo ambapo alijeruhiwa kwa risasi katika miguu yake yote miwili. Hivi sasa Bwana Vedastus amelazwa katika hospitali ya Aga Khan, Nairobi na anendelea kupatiwa matibabu na hali yake inaendelea vizuri.


Tuesday, September 24, 2013

VIDEO: WATOTO WAOANA.. YOTE HAYO NDANI YA JOYCE KIRIA WANAWAKE LIVE LEO.

Leo saa tatu kamili usiku utashuhudia watoto wakioana... ni watoto kabisa kama ulikuwa unasikia tu hizi story leo ndani ya Joyce Kiria Wanawake Live utapata kushuhudia hilo... then tutakutana hapa hapa kuchangia maoni yenu. Saa tatu usiku ndani ya EATV ni yote haya. 

Monday, September 23, 2013

MH WAZIRI MKUU; MAMA KIJO BISIMBA LEO USO KWA USO NA MTUHUMIWA WAKE MIZENGO PINDA

Waziri Mkuu Mizengo Pinda alitoa sifa kwa Shule ya waschana Weruweru kwamba ni  moja kati ya shule zilizotoa wanawake wa shoka hapa nchini Tanzania.
Katika mazungumzo hayo alisema kuwa hakujua kama mlalamikaji kwenye kesi inayomkabili yeye (Mh Pinda)  kwamba alisoma Weruweru. kesi ambayo ni ya kiKatiba aliyofunguliwa na shirika la Sheria na Haki za Binadamu ambalo linaongozwa na Mama Hellen Kijo Bisimba. kesi hiyo inahusu tamko alilolitoa Mh Waziri Mkuu la wananchi kupewa kipondo 

Wanageni waliohudhuria ghafla hiyo walishangilia kwa nguvu baada ya Mh Waziri Mkuu Mizengo Pinda kusema: Kesho waandishi wa habari hawana tabu ya vichwa vya habari kwenye magazeti kwa sababu wataandika ya kwamba ''USO KWA USO NA MTUHUMIWA'' Kama picha inavyozungumza...
Mh Waziri mkuu akifungua rasmi Shirika lililoanzishwa na Alumni wa Weruweru
Mh Waziri Mkuu Pinda akiskiliza Lengo la kuanzishwa kwa hiyo Taasis ya wana Alumni wa Weruweru
Mh Waziri mkuu akielekea kwenye tukio la harambee ya Weruweru
Mr and Mrs Mtei wakienda kutoa mchango wao katika shuguli ya miaka 50 ya Weruweru
Baadhi wa wadau wakiwa kwenye foleni ya kutoa mchango wa kuendeleza Elimu kwenye shule ya weruweru
Liliani mbowe mwana Alumni wa weruweru akitoa mchango... picha zaidi zinakuja

Saturday, September 21, 2013

PICHA: SHEREHE YA MIAKA 50 YA SHULE YA WERUWERU

Ni picha mbalimbali za Tukio la kusherekea miaka 50 ya shule ya Weruweru.... Waschana wa zamani wakiingia shuleni hapo na waschana wa sasa wakiwapokea kwa furaha.... 
Waschana wa weruweru wakifurahi na mama yao Mama Kamm.....

PICHA: MATUKIO YA LEO ASUBUHI DAKIKA CHACHE KABLA YA KUELEKEA KWENYE ENEO LA TUKIO WERUWERU

Keki ya kuwakaribisha wana Weruweru  asubuhi ya leo hapa kwa MAMA CLEMENTINA FOUNDASHION
Wanalishwa kutokana na mwaka waliomaliza shule weruweru... waliomaliza miaka ya 60 mpo?
Keki time, waliomaliza miaka ya sabini?
Waalimu wetu?
Keki time...Wanaume Live?
Picha ya kumbukumbu
Safari inakaribia kuanza
Safari ya kuelekea Weruweru ndo hiyooo.....Kwa matukio zaidi endelea kutembelea ukurasa wetu.... hiyo ni trela picha kamili yaja
Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...